Arsenal yaondoka na alama tatu muhimu baada ya kuilaza Nottingham Forest ugenini
Katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) jioni ya leo Jumapili, Arsenal wamepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Nottingham Forest, shukrani kwa goli la jioni kutoka kwa Noni Madueke. Bao hilo limeipa Arsenal alama tatu muhimu sana katika dimba la City Ground. Mchezo huo ambao kwa kiasi kikubwa haukuwa na mashambulizi mengi ya kusisimua, uliamuliwa katika dakika ya 80 baada ya shuti la Madueke kumgonga mchezaji wa Forest na kutinga nyavuni.